WAZAZI TWAPASWA KUWA KARIBU NA WATOTO
Sasa imekuwa ni jambo la kawaida kusikia habari za kusikitisha kwenye magazeti na vyombo vya habari, inatisha sana. Wazazi twapaswa kuwa waoga sana na ulimwengu huu wa sasa.
Kuna familia ambayo ilijaliwa kuwa na watoto wawili wa kike wenye akili sana na ilikuwa ni familia yenye furaha. Binti zao walikuwa wanafanya vizuri sana katika masomo yao na walimu waliwapenda sana. Wazazi wao walikuwa na upendo mkubwa kiasi hawakutaka mabinti zao wawe na mazoea na vijana wengine wa jirani kwa hiyo muda mwingi walikuwa wakirudi shule wako ndani tu na hawaruhusiwi kutoka hii ilikuwa ni katika kuwalinda na vijana wabaya. Wakiwa nyumbani walikuwa wanapenda kushinda chumbani na wazazi waliona kuwa binti zao wanaadabu sana kwa kukaa ndani.
Usiku mmoja waliamshwa na sauti kubwa ya kilio kutoka chumba cha mabinti zao. Walivyoenda huko walikuta binti yao mmoja amelala chini na ameloa damu wakasogea kumuangalia kuwa amepatwa na nini. Wakakuta katika uke wake kuna "test tube", binti yao mdogo amesimama pembeni mtupu hakuwa na neno la kueleza. Wakajaribu kuitoa ila ikavunjika, kwa hiyo wakamkimbiza hospitali lakini hali ilikuwa mbaya maana alikuwa anatoka damu sana, na bahati mbaya binti akafariki. Binti mdogo alipoulizwa, akajibu kwa sauti ya huruma "tulikuwa kila siku tunafanya hivyo nyumbani kwa sababu tunawaona wasichana wenzetu wakifanya hivyo shule, kwa hiyo tukajua kuwa tuko sawa kwa kuwa hakuna aliyekuwa anaongea nasi juu ya hilo" (akimaanisha wazazi wao). Kwa kuwa alishindwa kuvumilia maumivu ya kuondokewa na dada yake alipofika nyumbani akajinyonga chumbani kwake. Wazazi wale waliwakosa mabinti zao wapendwa na wenye akili.
Wazazi tunapaswa kukaa na watoto wetu na kuongea nao juu ya mambo mbali mbali yatokeayo kwenye jamii. Watoto wawe marafiki zetu ili wawe huru kuuliza lolote limkwazalo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment